Kira Kirami aelezea jinsi ZFU kinavyowaweka wasanii wa Zanzibar kuwa na Umoja

0

Rapa wa kundi Zee Town Sojaz, Kira Kirami amesema kuwa toka kianzishwe chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Z.F.U) kumekuwepo na ushirikiano mzuri kati ya wasanii Zanzibar katika kupeana sapoti.

kira

Akizungumza na Zenji255 Kira anasema kuwa chama cha wasanii Zanzibar kimefanya mapinduzi makubwa sana katika kuwaweka wasanii na sanaa yao pamoja japokuwa kuna matatizo madogo madogo lakini ilivyokuwa mwanzo na sasa hivi ni tofauti.

“Kiukweli zamani tulikuwa tunaona kabisa kumpa sapoti mwenzangu unaona kama unamkuza yeye tu tulikuwa hatujui nini tunafanya. Lakini sasa hivi umoja wetu umesaidia sana kwani unajua kabisa kama mimi nikimsaidia mwenzangu na mimi nitasogea ni kitu kizuri sana” Alisema Kira Kirami.