‘Kimya changu katika muziki ni kutokana na kubanwa kwa masomo’ – I.T

0

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar, Iddy Thabit El Maamiry maarufu kama I.T amerudi tena na wimbo mpya baada ya kukaa kimya kirefu ambacho kiliwafanya mashabiki wake wajiulize ukimya wake.

it2

Akizungumza na Zenji255 Msanii I.T amesema sababu za yeye kua kimya muda mrefu katika sanaa ya muziki kutokana na kubanwa na masomo pamoja na kuitumikia jamii Kuhusiana na mabadiliko mbalimbali yanayohusiana na muziki. “Najua kua kuna vijana wengi sasa hivi wanafanya vizuri katika muziki. Lakini mawazo yao wanadhani sisi watu wazima hatuwezi kufanya kama wao, kwahiyo mimi nimeonyesha kua tunaweza kufanya zaidi ya wao wanavyofanya. Ukiusikia wimbo wangu mpya utakubaliana na mimi pia nimepanga kuachia ngoma mbili kwa pamoja Bado navumilia na Moyo” Alisema I.T

Bado navumilia ni wimbo ambao I.T ameuachia hivi karibuni na umetengenezwa katika studio ya Saigon Record chini ya mtayarishaji anaefahamika kwa jina la Katuli.

 I.T alimalizia “Ukiondoa nyimbo ya talaka na lady ambazo ziligusa moyo wangu na ndio maana zilifanya vizuri sana. Wimbo wangu huu mpya wa bado na vumilia ni wimbo mwingine ambao ni true story.”