Khamis HK azungumzia project zinazokuja baada ya uzinduzi wa filamu ya ‘The Dream’

0

Meneja wa lebo ya Goodfather Music, Khamis HK amesema kwa sasa hivi wanajiandaa kuzindua filamu mpya iitwayo ‘The Dream’ na baada ya hapo kuna project nyingi zitafuata.

Khamis HK

Akiongea na Zenji255 HK amesema kuwa lebo ya Goodfather Music ikishirikiana na studio Mi8 kwa sasa zipo katika maandalizi baada ya uzinduzi wa filamu ambao utakaofanyika Januari 28, katika ukumbi wa Ngome Kongwe vile na baada ya hapo utafuatiwa na uzinduzi wa kampuni ya GoodFather Music.

“Baada ya uzinduzi wa filamu Januari 28, mwezi unaofuata (Februari) tutafanya uzinduzi wa lebo ya Goodfather Music pamoja na kuwatambulisha wasanii wapya ambao tumewasaini na idadi yake wapo wasanii nane. Kikubwa tunachowaomba wadau wa muziki na filamu kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa filamu kwani mambo mengi na mastaa wengi watakuwepo” amesema HK.