Kelele za mashabiki zamkasirisha Justin Bieber na kuondoka jukwaani

0

Justin Bieber aliondoka katika jukwaa la tamasha yake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati anapoimba.

justin bieber

Wakati wa tamasha zake tatu zilizopita katika mji huo ikiwa miongoni mwa ziara yake ya dunia nzima mwanamuziki huyo alisema : Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi munayonipa na nathamini ukarimu wenu.Lakini kelele munazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe.Tafadhali na ahsanteni.Sidhani ni muhimu ninapojaribu kusema kitu na nyinyi munapiga kelele.

Na mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele zao aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa,huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.

Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha yake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.

”Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho ,munajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana”.