Kashiru Salum aelezea utofauti wa soka la ufukweni na la kawaida

0
kashiru

Mfungaji bora wa ligi kuu ya Soka la Ufukweni Zanzibar Kashiru Salum ambae kwa sasa anacheza timu ya Kijichi katika ligi kuu soka ya Zanzibar ameelezea tofauti ya Soka la Ufukweni na soka la kawaida

kashiru

Akiongea na Zenji255 Kashiru amesema kuwa kwa soka la ufukweni hakuna tofauti sana lakini kubwa analoliona geni kwa upande wa soka la kawaida ni idadi ya watu, kwani soka la ufukweni idadi ni watu 4 na soka la kawaida watu 11.

“Beach soccer kiukweli lazima utumie nguvu nyingi kutokana ni mchangani tunacheza na akili nyingi kutokana urefu wa kiwanja ni mdogo sana kiasi ukipiga kidogo tayari ushatoa mpira nje. Vile vile mashabiki wa soka la kawaida wana hasira na makelele sana kiasi kwamba unakosa amani kuliko soka la ufukweni ugumu wa mchezaji kwa mashabiki unaonekana” Amesema Kashiru

Imetayarishwa: Ali M. Khamis