Jay Z aweka dau la kuinunua albamu ya Prince inayotarajiwa kuingia sokoni

0

Rapa kutoka Marekani Jay Z ameripotiwa kuwa anataka kuinunua albamu ya Marehemu Prince ambayo inatarajiwa kuingia sokoni.

jay z

Kutokana na mtandao wa TMZ imeeleza, Jay Z alionana na ndugu wa Prince, Tyka akiwa na mumewe Maurice Phillips wiki kadhaa zilizopita na kujadiliana kuhusiana na dili hilo. Imeripotiwa kuwa aliwasafirisha wapenzi hao kwenda New York kwa ajili ya mkutano huo.

Vyanzo vya ndani vimesema kuwa Jay Z alitoa ofa ya dola milioni 40 (bilioni 86,800,000,000 za Tanzania). Hata hivyo, Tyka amesema kuwa hana haki miliki zote za kusaini dili hiyo. Ila inatakiwa iwe na maridhiano yote kutoka kwa ndugu pamoja na uongozi wa Prince.