Jay Murder ajibu tetesi za kuwa Tongwe yaachana na Hip hop na kufanya Bongo Fleva

0

Mtayarishaji kutoka katika studio ya Tongwe Records, Jay Murder aelezea kuhusiana na tetesi za kuwa studio hiyo sasa haifanyi tena kazi za Hip Hop baada ya kuonekana kwa sasa wameekeza sana kwenye Bongo Fleva.

11249801_1564634097137306_774724883_nAkizungumza na Zenji255 Jay amesema kuwa kwa sasa muziki umebadilika na studio hiyo imeamua kufanya muziki wa bongo fleva kwa sababu muziki wa sasa upo kwenye biashara zaidi ila muziki wa Hip Hop utaendelea kubakia Tongwe.

“Tongwe ni kisiwa cha Hip Hop na sisi bado tunafanya Hip Hop lakini Joff Masters ni producer mwingine wa Tongwe na yeye ndie anaefanya sana muziki wa bongo fleva. Kuna kazi nyingi mpya za wasani kama Cyrill Kamikaze, Jose Mtambo, Roma na zipo nyingi zinakuja hivi karibuni ambazo zinatokea Tongwe” Alisema mtayarishaji Jay Murder