Jay Dee amtaja director aliyesimamia video yake ya ‘Ndi ndi ndi’

0
jay dee

Lady Jaydee ameweka hadharani kuwa Justin Campos ndiye aliyeongoza video ya wimbo wake mpya, ‘Ndindindi.’

Staa huyo amepost video Instagram inayomuonesha Justin akiwa na mke wake Candice Campos kueleza walivyokutana.

“Nilikutana na Justin Campos Kwa Mara ya Kwanza 2006 Wakati Tunafanya Video ya Njalo Nilioshirikiana na kundi la South Africa Linalojulikana Kama Mina Nawe, Justin Ndio alikuwa Director wa Video Hiyo Baada ya Miaka 10 tumefanya kazi tena 2016,” aliandika Jaydee.

 

“Dunia Duara tunazunguka Tunarudi tena tunakutana #NdiNdiNdiMusicVideo #ThisComingThursday #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea #KaaTayariKuipokea,” aliongeza.