Jaka B amtaka Buyubaya amtafute mlinzi wa kumlindia mkewe

0

Msanii na producer wa Gun Records Jaka B ametoa malalamiko yake ya kuwa yeye sio mlinzi wa kumlinda mke wa Buyubaya Mtabiri.

buyubaya

Akizungumza na Zenji255 Jaka B amesema kuwa Buyubaya ni mtu wake wa karibu kiasi kwamba mambo mengi huwa wanafanya pamoja lakini Jaka B anasema wivu wa mkewe huwa unavuruga wakati wa kazi.

“Mimi mwenyewe nina mke na anaelewa harakati zangu lakini kwa buyubaya itabidi atafute mlinzi wa kumlinda mkewe. Tukienda kwenye show huwa anamchukua mkewe¬† na ubaya zaidi pale akimuona Mtabiri ametoka na kachelewa kurudi naanza kuulizwa mimi”. Amesema Jaka B

Kwa upande mwingine Buyubaya mtabiri nae amesema “Mke wangu ni mmoja wa mashabiki wangu na huwa mara nyingi hupenda kuwa nami ninapoenda kufanya shoo. Kwahiyo Jaka B si mlinzi wa mke wangu isipokuwa tunapokaa VIP, wasanii na mke wangu huwepo. Juu ya hilo naomba Jaka B aniombe msamaha kwani amenikosa”.