J Combat kuandaa tamasha la Zinduka Dance

0

Kundi lililoshinda nafasi ya pili katika mashindano ya dance 100, J Combat lina mpango wa kuandaa tamasha la Zinduka Dance mwakani 2017.

j combat

Akizungumza na Zenji255 msemaji wa kundi hilo amesema kuwa Zinduka Dance ni tamasha ambalo litakalokuwa linatafuta vipaji vya kucheza na linatarajiwa kufanyika mwezi wa pili mwakani baada ya tamasha la Sauti za Busara kuisha.

“Unajua Zanzibar vipaji vipo vingi sana na ndio maana tukaamua kuanzisha hili tamasha. Kwa sasa bado hatujapata wadhamini ila tunahitaji wadhamini, na lengo letu ni kunyanyua vipaji vya Zanzibar ili baadae tupate wawakilishi ambao watakaoshiriki katika mambo mbali mbali katika kucheza na ndio maana tukalipa jina Zinduka Dance.” Amesema