Categories
E! News

Ivan azungumzia kuhusiana na shavu alilopata kupitia video ya ‘Komela’

Kama utakuwa unamkumbuka director Ivan aliyeongoza baadhi ya video za wasanii kutoka hapa hapa Zanzibar zikiwemo video 2 za Rico Single, Chekecha na Yani Raha. Hivi karibuni Ivan amekula shavu la kushoot video mpya ya AY.

Ivan
Director Ivan akiwa location

Nafasi hiyo kwa Ivan ilitokana na video ya Dayna Nyange aliyoshirikiana na Bill Nas ‘Komela’. Ivan kwa sasa ameshafanya kazi ambazo zinafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya TV nchini na nje ya nchi zikiwemo kama Ghetto (Sholo Mwamba) na nyinginezo.

“AY ni kama ndugu yangu” Amesema Ivan “Kiukweli mungu ni mwema na ninashukuru mpaka hapa nilipofikia. Kuna kampuni kutoka Afrika ya Kusini wametaka kufanya kazi na mimi na vile vile kuna kazi hivi karibuni nitafanya na AY. kikubwa ni watu wasubirie mabadiliko ya kazi zangu” Amemalizia Ivan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.