Ison Mistari asaini mkataba mpya na Stone Town Records

0

Mkali wa wimbo wa ‘Kama Ngosha’, Ison Mistari hivi karibuni amesaini mkataba mpya na label ya Stone Town Records.

Mmoja wa wahusika wa label hiyo aliandika kupitia Instagram yake: Ison Mistari akiwa tayari kasaini mkataba wa kuwa na label ya Stone Town Records… Muziki mzuri karibuni

Zenji255 imemtafuta mmoja ya mhusika wa label hiyo, Kassim Omar (Mash Marley) na  kuzungumzia mkataba huo.

“Ison ni msanii anaefanya vizuri hapa Zanzibar na tayari tushakubaliana makubaliano na habari nzuri ni kwamba tayari kishatengeneza albam yenye nyimbo nane,” amesema Mash Marley.