Instagram kutumia nembo mpya

0

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee.

instagram

Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa.Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua.

Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika Instagram.

Mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014.

Wakati Instagram ilipoanza ,ilikuwa eneo la kukarabati na kusambaza picha,kampuni hiyo ilieleza. Miaka mitano baadaye,ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.

Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe. Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo.

Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita ,instagram iliambia Newbeat. Tulitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.

Source: BBC Swahili