“Imefikia wakati sasa wasanii wakongwe wa Zanzibar tuwasaidie vijana wapya mbinu za muziki” – Baby J

0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baby J amewaomba wasanii wakongwe katika tasnia mbali mbali ya sanaa visiwani Zanzibar kuwa wamoja na kuwasaidia vijana wachanga katika kusaidia taifa katika kazi mbali mbali za sanaa.

baby j

Akizungumza na waandishi wa habari, Baby J amesema kuwa Zanzibar ina wasanii wengi wakongwe wenye taaluma mbali mbali na itakuwa ni vizuri kwa serikali kushirikiana na wasanii kuwaweka sehemu moja na kuanza kutoa taaluma yao kwa wasanii wachanga.

“Serikali ikishirikiana na wasanii wa hapa Zanzibar na endapo wakafungua shule ya kuibua vipaji mbali mbali kama uchoraji, muziki, uchongaji na mengine mengi. Tunaweza kuifanya Zanzibar ikawa namba moja katika kukuza vipaji.” Amesema Baby J

Hivi karibuni Baby J aliyazungumza maneno hayo wakati akizindua foundation yake ambayo itakayokuwa ikisaidia wasanii wachanga visiwani Zanzibar hasa hasa upande wa wanawake, iliyofanyika katika Hotel ya Muruhubi Resort Mjini Magharibi, Zanzibar ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa muziki kutoka Zanzibar na Tanzania bara huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mh Yusuph Mohammed.