Huu ni wito kwa wasanii kutoka kwa Sauti za Busara

0

Je muziki wako unahusiana na Afrika, au nchi za bahari ya hindi?

Je muziki wako ni wa laivu? 

Je umevutiwa kupiga muziki mwezi ujao wa Februari Zanzibar? 

Kama unaweza kujibu ndio, ndio, ndio – basi endelea kusoma… 

Sauti za Busara ni tamasha lifanywalo kila mwaka mwezi wa Febrauri Zanzibar, huonesha muziki wa Afrika yote na kwengineko. Tamasha hilo limo kwenye mtandao wa CNN ilitoa orodha ya matasha 7 ya Afrika kuyaona ni lazima, Kwenye gazeti la Songlines la Uingereza limo kwenye matasha 25 bora ya kimataifa na mtandao wa kitalii wa Afro Tourism’s umeliingiza tamasha hili katika matasha 8 bora ya muziki. Na mwezi wa Februari 2015, BBC World Service imelitaja tamasha la Sauti za Busara kama ni ‘moja kati ya matukio muhimu na yenye kuheshimika barani Afrika’.

Kufahamu mengi na kutaka kujaza fomu ya maombi bonyeza Hapa