Huu hapa ni wito kwa wasanii katika tamasha la Sauti za Busara 2018

0

Tamasha la 15 la Sauti za Busara, ni moja kati ya matamasha bora Afrika, litafanyika tena Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 8 – 11 Februari 2018.

sauti za busara

Sauti za Busara 2018 litakutanisha vikundi 40+ kutoka barani Afrika na kwingineko kufanya maonyesho katika jukwaa tatu kwa siku nne mfululizo. Wasanii kutoka Nchi za kiarabu na ukanda wa Bahari ya Hindi wanakaribishwa kufanya maombi.
Maombi yanapokelewa mpaka tarehe 31st July 2017. Maombi yasiyokamilika au yatakayoletwa nje ya muda uliopangwa, hayatapewa kipaumbele. Kuomba ushiriki, tafadhali tuma mahitaji yote yaliyoorodheshwa hapo chini.

Bonyeza hapa kupata Fomu ya maombi

 • Maelezo/ Historia ya Msanii*
 • Nakala iliyotolewa karibuni* (tuma nakala 2 kwa njia ya posta, au nyimbo 3 kwa wetransfer/dropbox)
 • DVD ya maonyesho yako ya moja kwa moja (LIVE), au video kwa wetransfer/dropbox (kama itapatikana)
 • Picha 2* (zenye uwezo wa kuchapisha)
 • Mpangilio wa Jukwaa na Mahitaji ya kiufundi (kama itapatikana)

Nyaraka zitakazoambatanishwa lazima ziandikwe na kutumwa kwa barua pepe [email protected]
Maombi ya kuchapisha yatakayotumwa kwa njia ya posta yatapewa kipaumbele na lazima yatumwe anuani ifuatayo:
Journey Ramadhan
Busara Promotions
P O Box 3635
Zanzibar
Tanzania

Tafadhali andika kifurushi chako “Contents not for sale. For promotional use only”
Muda wa kupokea maombi ni tarehe: 31st July 2017

Kama utachaguliwa, tamasha litagharamia yafuatayo kwa wasanii na kiongozi mmoja:

 • Malipo ya onyesho
 • Pesa ya chakula
 • Malazi
 • Usafiri wa ndani utakapokuwa Zanzibar kwa ajili ya onyesho lako
 • Malipo ya viza, ambatanisha risiti
 • Pasi ya kuingia kwenye tamasha zima
 • Maelezo ya Kikundi kwa kitabu cha tamasha, taarifa za vyombo vya habari, tovuti na mitandao ya kijamii.