Huenda hapa ikawa ndio mwisho wa kundi la Wrong Turn

0

Kundi la ‘Wrong turn’ linaloundwa na wana hip hop wawili Ison Mistari na Chaby Six (Mashine) hapo ilionekana kushika masikio ya watu visiwani Zanzibar baada ya mmoja wao katika kundi hilo Ison kuamua kutoa taarifa ya kujitoa katika kundi hilo kupitia Instagram na kusema kuwa hataki tena mambo ya makundi.

Akizungumza na zenji255 Ison alisema “Kiukweli NimeĀ  We are so selfish kwa sababu kila mtu yuko busy na mambo yake na kila mtu ana angalia upande wake wa kufanya kazi kivyake lakini hakuna movement zozote zinashirikisha kundi yaani kwa lugha nyingi ni kwamba nimechoka kujipendekeza kwa Chaby.”

Na kwa upande mwingine Chaby Six nae pia alizungumzia kuhusiana na maamuzi aliyoamua rapper mwenzake kutokea kundi hilo alisema “Sijapata Taarifa yoyote kutoka kwake, isipokuwa nilipigiwa simu na kuambiwa kuhusiana na mwenzangu kujitoa na nilitafuta katika simu lakini hapokei. Kiukweli mimi sijapenda Alichokifanya, najua kila mtu ana maisha yake na mambo yake lakini kutangaza mitandaoni unaamanisha unataka kiki. Mimi siwezi kumzuia juu ya uamuzi alioamua ila namtakia kila la heri na maisha mema katika muziki wake.”

Tuutizame muziki wetu ulipo hapa visiwani na ‘wrong turn’ lilikuwa ni kundi lililokuwa linaleta changamoto Zanzibar kwa wasanii wengine wa Hip Hop. Ni matumaini makubwa sana ya Zenji255 kuwaona hawa jamaa wataelewana na kuendelea na umoja wao na kuuendeleza muziki wa Hip Hop hapa visiwani.

Angalia moja ya video ya kundi hilo la Wrong turn.