Hii hapa ni ‘suprise’ nyingine kutoka kwa Chidy Grenade ambayo huenda ikaachiwa karibuni

0

Wiki kadhaa zilizopita Zenji255 ilishawahi toa maoni juu ya wasanii chipukizi ambao watakaofanya vizuri kwa mwaka 2017 na kuweza kuutangaza muziki mbali zaidi, Chidy Grenade hivi karibuni amefunguka kuhusiana na ujio wake mpya ambao huenda akauachia hivi karibuni.

chidy

Akiongea na Zenji255 Chidy amesema kuwa alikua na ndoto kubwa sana katika muziki kukutana na mtayarishaji ambae alikuwa na hamu ya kufanya nae kazi katika muziki wake.

“Nahreel ndie mtayarishaji niliekuwa na-wish kufanya nae kazi” Amesema Chidy Grenade “Na tayari tushafanya hiyo kazi ila kwa sasa siwezi kusema nitaachia lini na wapi kwa ni suprise kwa mashabiki, kutokana na uongozi bado unafanya mipango mingine kabisa ambayo hata haiendani na kazi hiyo iliyokuwepo kwa Nahreel” Amemalizia Chidy Grenade.