Hii hapa ni ratiba kamili ya mashindano ya BE.TALENT

0

Mashindano ya kutafuta vipaji mbali mbali hapa visiwani Zanzibar ya BE.TALENT ambayo yameandaliwa na lebo ya muziki ya Stone Town Records pamoja na Fumba Town Development wametoa ratiba kamili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi 23 mwezi huu saa nne asubuhi katika ukumbi wa CCM VIP club (Maisara).

Akizungumza na Zenji255 mkurugenzi wa lebo hiyo Mash Marley, amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa na awamu mbili kwa raundi ya kwanza itafanyika CCM VIP club (Maisara) na awamu mbili kwa raundi ya pili ambayo itafanyika katika uzinduzi wa mradi wa nyumba mpya za Fumba Town Development zilizopo Fumba.

“Awamu ya kwanza itakuwa ni kutafuta washiriki ambao watatinga nusu fainali ambapo tumepanga zitakuwa siku mbili jumamosi na jumapili (23 na 24 Juni 2018) na majaji ni Baby Jay (Msanii wa muziki),  Ramadhan Journey (Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara), Salum Stika (Mwenyekiti wa chama cha waigizaji) na Mash Marley.” Amesema Mash.

Ameongezea kuwa “Nusu fainali na fainali itafanyika katika uzinduzi wa mji mpya huko Fumba ambapo raundi ya kwanza itakuwa Jumamosi 30 Juni na fainali itakuwa jumapili 1 Julai”

Fomu za usajili zinapatikana mlangoni siku ya tukio pale CCM VIP club Kuanzia saa nne asubuhi.