Hii hapa ni mipango mipya ya ZFU juu ya wanachama wake

0

Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zanzibar (ZFU) unafikiria kuandaa mipango maalum ambayo itakayoweza kuwasaidia wasanii na wanachama wake kwa lengo la kuwakomboa wakati wanapokumbwa na matatizo mbali mbali.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama hicho Mohamed Abdulla Laki siku ya Jumanne (Feb 28) akiwa na  Ujumbe wa Viongozi Wanne wa ZFU wakati wa mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ofisi ya iliyopo Vuga, Mjini Zanzibar.

Laki amesema kuwa ZFU ina mipango ya kuanzisha bima ya afya kwa wanachama wake kwani inakuwa aibu na masikitiko makubwa  pale  msanii ambaye ni kioo cha jamii anapoonekana akidhalilika wakati akitafuta huduma za matibabu kipindi anaposumbuiliwa na matatizo ya kiafya bila ya kupata msaada wa uhakika.

“Mpango wetu mwingine, chama kimepanga kuandaa tamasha la kuibua vipaji vya wasanii wapya  linalotarajiwa kuandaliwa na Chama hicho mwezi Septemba Mwaka huu. Wasanii watakaoonyesha uwezo mkubwa  siku hiyo watatunukiwa zawadi maalum ili kuwapa motisha wa kuendeleza vipaji vyao” Amesema Laki