Hii hapa ni 5 bora ya wana Hip Hop wenye mkwanja mkubwa Marekani

0
hip hop

Jarida la Forbes limetoa orodha mpya ya wasanii wa hip hop wenye fedha zaidi. Ambapo katika orodha hiyo P. Diddy akiwa ameshikilia nafasi ya kwanza kwa kipindi cha miaka 2.

Hii hapa Top five:-

  1. P. Diddy (Dola Milioni 750)

Baada ya kuachilia Mixtape yake ya MMM (Money Making Mitch), Diddy pia ana bidhaa ambazo zinamuingizia fedha kama vile Ciroc Vodka, Revolt na Nguo za Sean John.

2. Dr. Dre (Dola Milioni  710)

Kutokana na mauzo ya Head phone zake za  Beats By Dre kufanya vizuri, vile vile Filamu ya Straight Outta Compton kuwa na mauzo makubwa duniani.

3. Jay Z (Dola Milioni 610)

Tidal mtandao anaomiliki unashuhulika na kazi za wasanii ambao una watumiaji Milioni 3 wanaolipa kununua kazi za wasanii katika mtandao huo.

4. Bird Man (Dola Milioni 110)

Mmiliki wa lebo ya Cash Money safai hii amepanda nafasi kutokana na kufanya vizuri katika mauzo ya kazi zinazotoka katika lebo yake.

5. Drake (Dola Milioni 60)

Kwa mara ya kwanza Drake ameingia katika list hiyo baada ya mauzo mazuri ya Albamu yake na show anazofanya. Vile vile anaingiza fedha kutokana na malipo ya kampuni ya Nike, Apple na Sprite