GoodFather Music huenda ikamsaini Abramy

0

GoodFather Music Entertainment kama inavyofahamika na wadau wengi wa burudani ni management ambayo iliasisiwa na mwanaharakati wa muziki kutoka visiwani Zanzibar anayefahamika kwa jina la Khamis HK.

hk_abraKwa kiasi kikubwa uongozi huu umefanikiwa kuwasaidia baadhi ya wasanii hapa Zanzibar na tena sio wasanii wa muziki wa kizazi kipya tu bali hata wa maigizo.

Lakini kwa siku za hivi karibuni kupitia Instagram ya uongozi huo iliandikwa taarifa ambayo inamhusisha msanii kutoka katika kiwanda cha Zenji na Bongo Flava, Abramy kuwa yupo katika mazungumzo na uongozi huo kwa ajili ya kumsimamia kazi za muziki wake. Tetesi ambayo iliasisiwa na boss wa management hiyo ya GoodFather Music, Khamis HK.