Fraga aelezea tofauti ya uimbaji wa wasanii wa Zenji Fleva na Bongo Fleva

0

Mtayarishaji kutoka studio ya Uprise Music, Fraga ameelezea utofauti uliokuwepo kati ya wasanii wa Zenji Fleva na Bongo Fleva kuwa wasanii wengi wa Zanzibar uimbaji wao una mahadhi ya kiarabu.

fraga

Akiongea na Zenji255 Fraga amesema kuwa Zanzibar ni visiwa vilivyotawaliwa na waarabu na historia ya muziki wao umetokana na mahadhi ya kiarabu, na wasanii wengi uimbaji wao uko sawa na mahadhi hayo.

“Ila kuna wasanii ambao mimi nimefanya nao kazi naona wapo tofauti kidogo kama Smile na Abramy, wanajaribu kufanya vitu tofauti na hayo mahadhi. Ila kwa wasanii wengine naona wanafanana na uimbaji wa Taarab au mduara, ila ni nzuri kwa utambulisho wa muziki wa nyumbani” Amesema Fraga.