Firmino ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

0

Mchezaji wa Liverpool Roberto Firmino ameshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi baada ya kukamatwa mkesha wa siku ya Krismasi.

firmino

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa baada ya gari lake kusimamishwa katikati mwa Liverpool mapema siku ya Jumamosi ,polisi wamesema.

Mchezaji huyo wa Brazil anatarajiwa kufikishwa mbele ya hakimu wa Liverpool mnamo Januari 31.

Firmino atawasilishwa mahakamani siku ambayo timu yake itakabiliana na Chelsea katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ilimsajili mchambuliaji huyo kutoka Hoffenheim kwa kandarasi ya miaka mitano iliogharimu kitita cha pauni milioni 29 mwezi Juni.

Alicheza katika ushindi wa wiki iliopita dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park.

Liverpool imesema kuwa haitazungumzia swala hilo hadi pale hatua hiyo ya kisheria itakapokamilika.

Chanzo: BBC Swahili