Categories
E! News

Fanny apata shavu la kufungua Fiesta Mwanza

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea visiwani Zanzibar, Fanny amepata nafasi ya kushiriki katika ufunguzi wa Tamasha la Fiesta linalosimamiwa na kampuni ya Clouds Media chini ya redio ya Clouds FM.

Kwa mwaka 2019 Fiesta itafanyika katika mkoa wa Mwanza na ambapo Fanny atakuwa katika list ya ufunguzi huo.

Akizungumza na Zenji255, Fanny amesema anafuraha kubwa sana kupata nafasi hiyo kwani kwa muda mrefu sana muziki wa Zanzibar kwenye tamasha la Fiesta haukusikika na kwa mkoa wa Mwanza ni pahala pake kuupeleka muziki wa Zanzibar.

“Hakuna kitu kizuri kama kuiwakilisha sehemu unayotokea unapokuwa ugenini, na mimi nafurahi sana kuwa nitakuwa wa kwanza kuutangaza muziki wa Zanzibar urudi katika ile nafasi yake ya zamani ambayo ilisahaulika kwa muda mrefu katika Fiesta” – Fanny

Fanny ameongeza kuwa “Nawaahidi wazanzibari na wasanii wenzangu kwamba sitowaangusha na nitahakikisha bendera ya Zanzibar inapepea kisawasawa. Kikubwa tupeane sapoti kwani hakuna kitu kizuri kama tukiwa pamoja na kushirikiana kupeleka muziki wetu duniani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.