Fainali ya ‘Insha Competition 2016’ kufanyika leo Juni 5

0
Jumla ya wanafunzi 20 waliongia katika hatua ya 20 bora wanatarajiwa kushirikii katika shindano la Insha competition lililo andaliwa na The voice of the voiceless Foundation upande wa Unguja, Zanzibar kwa kushirikisha shule za sekondari na kwa wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne.
2
Kwa mujibu wa waandaaji wa Insha Competition, Bwana Omary Amiry Mdogwa amesema kuwa tayari maandalizi yote yamekamilika na shindano hilo linatarajiwa kufanyika ndani ya ukumbi wa Hotel ya Double Tree by Hilton mjini Unguja kuanzkia saa 3 hadi mchana huku wadau mbalimbali wakialikwa kushuhudia tukio.
Aidha, kwa mwaka huu shindano hilo limedhaminiwa na ComNet Tz , Printplus ,Tropical Air ,Double Tree Hotel, Bomba Fm na wengine wengi.
Majaji ya shindano hilo ni walimu wa shule mbalimbali za Sekondari. Hili ni la mara ya kwanza ambapo jumla ya washiriki walikuwa 120. Katika hatua ya awali hadi sasa walichujwa na kubaki 20 ambao wameingia 20 bora.
1
Katika fainali hiyo washindi watatu wanatarajiwa kupatikana.