Fahamu: Mambo 5 katika Mwezi wa Ramadhani unapokuwa Zanzibar

0

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi muhimu sana katika mwaka kwa waislamu ndani ya Zanzibar na duniani kote. Kipindi hiki cha mwezi huu hutokana na kuandama kwa mwezi katika mwaka wa kiislamu, uliyokuwa tofauti na kalenda ya kimagharibi.

kanga

Visiwa vya Unguja na Pemba ni visiwa vyenye asilimia nyingi ni waislam na katika kipindi hiki kama wewe ni mgeni ndani ya Zanzibar basi ni vizuri kuyafahamu mambo 5 unapokuwa Zanzibar ili uweze kufurahia ukaaji wako.

  1. Wakati wa mchana mara nyingi sehemu zinazouzwa vyakula huwa zinafungwa. Kuna baadhi ya sehemu tu ndio huwa wazi kutokana watalii wanaokuja kutembelea Zanzibar.

2. Kuwa mpole.

3.Kuwa Muangalifu. Usinywe, usile wala kuvuta sigara ovyo mitaani, sio jambo jema ukionekana unakunywa au kula hasa hadharani. Hii ni muhimu sana hasa hasa kipindi hiki cha Ramadhani

4. Usione tabu kuuliza maswali kuhusiana na uislam. Wazanzibari wengi huwa na furaha wanapozungumzia kuhusiana na dini ya kiislamu na kuielezea kwa wageni, Hasa hasa nguzo tano za Uislam na sababu za kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

sikukuu25. Sheherekea sikukuu ya Eid. Baada ya mfungo wa mwezi mzima wa Ramadhani, waislam wote duniani husheherekea sikukuu ya Eid-el-Fitr ambapo huwa inasheherekewa katika viwanja mbali mbali pamoja na kuwatembelea ndugu na marafiki. Kila mtu huwa amependeza kwa mavazi mazuri na vyakula vya kila aina. Ni sehemu nzuri kuwepo.

Source: Mambo Magazine