FA yailipa Chelsea Paundi milioni 150.8

0

Klabu ya soka ya Chelsea imelipwa paundi milioni 150.8 na chama cha soka cha England FA baada ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2016-17.

Msimu wa 2015-16 ulishuhudia ongezeko kubwa kwa mkataba wa matangazo ya Televisheni ukitoa takriban Paundi bilioni 2.4 kwa timu 20 zaidi ya msimu uliopita zilipolipwa Paundi bilioni 1.6.

Timu iliyoshika mkia kabisa Sunderland imepata Paundi milioni 93.471. Fedha hizo zinatokana na matangazo ya Televisheni, mikataba ya kibiashara sambamba na zawadi.