England yatoka sare na Urusi Euro 2016

0

Michuano ya kombe la Euro kwa hapo jana ilikuwa ni mchezo kati ya timu ya taifa ya England dhidi ya Urusi, huu ni mchezo ambao ulikuwa unatazamwa na watu wengi kwa Afrika.

england

England walicheza mchezo ambao hadi dakika 90 zinamalizika walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 53, wakati Urusi walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 47, licha ya kuwa England walikuwa wamiliki mpira walilazimishwa sare ya goli 1-1.

Kwa hali ya mchezo ilivyokuwa England walikuwa wanaonekana kama wataibuka na ushindi kwani hadi dakika ya 89 walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 lililofungwa na Eric Dier dakika ya 73 kwa faulo, ila hali ilibadilika dakika ya 90 baada ya Vasili Vladimirovich kuisawazishia goli Urusi.

Angalia matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa hapo jana.

tr