England na Scotland waingia matatani FIFA baada ya kufanya maombolezo uwanjani

0

Bodi ya shirikisho la soka duniani, FIFA imetoa tamko la kufungua kesi juu ya taratibu za kinidhamu dhidi ya wachezaji wa timu mbili za Uingereza na Scotland baada ya timu hizo kuvaa vitambaa begani kama ishara ya maombolezo na kumbukizi kwa wachezaji wenzao ambao walipoteza maisha vitani.

england

FIFA imesisitiza kwamba kitendo kama hicho kinaangukia katika marufuku zifananazo na masuala ya kidini, masuala ya kisiasa ama kauli binafsi katika mechi za timu za taifa.

Kwa pamoja timu ya Uingereza na Scotland ambazo ziko chini ya shirikisho la soka inaarifiwa kwamba wakati wa maadhimisho ya usiku wa ijumaa iliyopita za kufuzu Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa Wembley kwamba walikuwa tayari wamejiandaa kukabiliana na matokeo ya kukaidi sheria za shirikisho la soka duniani FIFA .Mashirikisho yote mawili yanaweza kukabiliwa na faini.

Chanzo: BBC swahili