Dully Sykes baada ya ‘Inde’ huu ndio mpango wake mpya

0

Msanii Dully Skyes amesema kuwa baada ya ngoma yake ya ‘Inde’ kufanya vyema na kupokewa vizuri sehemu mbalimbali mpango wake sasa ni kuingia studio tena na kufanya collabo nyingine na msanii mwingine.

dully sykes

Dully amefanya kazi ya ‘Inde’ ambayo kwa sasa anafanya vizuri akiwa ameshirikiana na Harmonize kutoka WCB.

Dully Sykes amesema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo, Dully Sykes anadai kwa sasa kila kazi atakayoachia itakuwa ni ya kushirikiana maana ameshafanya sana kazi nyingi akiwa peke yake.

‘Nashukuru Mungu ‘Inde’ imefanya vizuri na inafanya vizuri nimepata mrejesho kutoka kwa watu mbalimbali sehemu mbalimbali hivyo naweza kusema kazi hii imefika dunia nzima, maana nimekuwa natumiwa sana ujumbe kwa lugha za watu mimi naelewa neno lile Inde tu. Lakini leo naingia tena studio kufanya kazi nyingine na hiyo pia nitashirikiana na msanii mwingine sitaki kumtaja sasa ila sasa itakuwa ni mwendo wa kushirikisha maana nimefanya sana kazi za kwangu pekee yangu, nataka niweka uwiano sawa” alisema Dully Skyes

Mbali na hilo Dully Skyes amefafanua kuwa kwa sasa yeye hayupo WCB Wasafi na wala hajasaini mkataba na WCB bali wale ni watu wake wa karibu ambao amekuwa akishirikiana nao katika kazi’

“Sipo WCB Wasafi na wala sijasaini wasafi ila nipo nao karibu na nafanya kazi nao karibu, mpaka sasa nimefanya kazi zaidi ya sita na Diamond Platnumz na sifikirii kama zitatoka saizi” alisema Dully Skyes