‘Dobi ni wimbo wa AT, Nassir Hawezi kutunga nyimbo’ – Producer Fraga

0
fraga

Na Mkali Nesta

Msanii na mtayarishaji wa studio ya Uprise Music, Fraga amefunguka kuhusiana na wimbo mpya ulioimbwa na Nassir Vanillah uitwao ‘Dobi’ ni wa AT na si Nassir Vanillah.

Akizungumza na Zenji255 Fraga amesema “Unajua nassir hajui kutunga sio muandishi mzuri ngoma zake zote alizoimba nimeandika mimi, kwa hiyo kaona hana cha kuimba akaamua kuiba wimbo wa Dobi, na ukweli ni kwamba Dobi ni wimbo wa AT”

Fraga hakuishia hapo aliongezea kuwa “Unakumbuka kipindi Nassir alipopata majanga yake, AT aliamua kumchukua na kwenda kuishi nae na aliandika hiyo ngoma kwajili ya kumtangaza nassir kimuziki ili apate kufahamika zaidi lakini ilifika time walishindwa kuelewana, so AT akamwambia Nassir hiyo ngoma aachane nayo na arudi zenji, wimbo AT ataufanya mwenyewe”

Fraga kwa upande wa pili alisema AT tayari ameshausajili wimbo huo katika Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na akasema kwa sasa Nassir afanye promotion kwa upande wake na sisi tuna fanya promotion kwa upande wetu mashabiki ndio wanaojua upi muziki mzuri.

Sikiliza hapa wimbo wa DOBI alioimba AT akiwa Fraga

http://www.audiomack.com/song/zenji255/dobi