‘Sina Bifu na Birdman pamoja na Cash Money’ – DJ Khaled

0

Baada ya Rick Ross kusema kwenye wimbo wake wa “Idols Become Rivals” kuwa Birdman amemsababishia maumivu sana Dj Khaled na kumtapeli pesa zake

dj khaled

Dj Khaled maarufu sana kwa kuleta wasanii pamoja kwenye colabo kubwa amefunguka Kwenye kipindi cha BreakFast Club kusema kuwa yeye hana bifu na Birdman au Cash Money, wao ni marafiki.

“Nataka niwe wazi hapo, naomba sana watu waweze kuzungumza na kuweka mambo sawa Nina mapenzi ya kutosha kwa Birdman na Slim, walinipa nafasi na nashukuru kwa yote waliyofanya, haijalishi kilichotokea baadae” Amesema DJ Khaled

Khaled alivyoulizwa kuhusu utapeli wa Birdman, alisita kuongelea biashara zake kwenye radio ila alikiri kuwa anawapenda wote akimaanisha, Rick Ross, Birdman na Slim.

Album mpya ya Khaled #Grateful inatoka June 23.