‘Director kakutongoza na umemkatalia, basi ujijue kazi huna au utashushwa thamani’ – Sophie

0

Kuna changamoto nyingi wasanii wa kike wanaocheza filamu wanazipata hapa visiwani ikiwemo kuhusishwa kimapenzi na viongozi au waigizaji wenzao, na endapo utakataa unaweza hata kwenye filamu au lile kundi husika ukafukuzwa.

sophie

Hayo ameyazungumza mcheza filamu wa kike kutoka hapa Zanzibar, Sophie. Amesema kwa upande wake ilishatokea katika kundi lao, alipokabidhiwa tunzo ya kuwa msanii mwenye heshima na muadilifu katika kundi lao.

“Waigizaji wenzangu walinuna mpaka ikafikia hatua hatusemeshani wakati tunapomaliza mazoezi, na mimi sikujua nini kinaendelea ila niliipokea ile tunzo. Baada ya siku kadhaa, kiongozi wetu akanifuata na kuniambia kwamba ananitaka kimapenzi na nilipomkatalia alinishusha thamani na kunitolea maneno machafu na kufukuzwa kabisa. Kiukweli inakatisha tamaa kwa wanawake” Amesema Sophie.