Diamond Platnumz atajwa kuwania tuzo ya ACI-AWARDS nchini Marekani

0

Mtanzania Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo za African Culture Image (ACI) Awards zinazofanyika kuwatunza waafrika popote walipo duniani.

Diamond ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyetajwa kuwania tuzo hizo zilizotawaliwa na wasanii kutoka Nigeria.

Diamond anawania kipengele cha Male Artist of the Year akichuana na wasanii kama Wizkid, Davido, KCEE, Patoranking na Olamide.

Tuzo hizo zitatolewa katikati ya mwaka huu huko Atlanta Georgia, Marekani. Jinsi ya kupiga kura tembelea http://www.aciawards.com/music/