Chambuso akanusha Yamoto Band kusambaratika

0

Msimamizi wa Yamoto Band, Chambuso, ameweka wazi kuwa fununu zinazoendelea juu ya kundi hilo la muziki kutoelewana kwa sasa siyo za ukweli.

yamoto

Akizungumza na eNewz, Chambuso amesema kuwa Yamoto Band kwa sasa wamekua na kwamba wana uamuzi wa kufanya vile wanavyo jisikia na suala la nyumba walizojengewa ni za kwao hata kama hawataendelea kufanya kazi na Said Fella.

“Tukianza nao walikuwa watoto kuna vitu tulikuwa tukiwazuia wasifanye hata kuzurura mitaani kuna kipindi tulikuwa tukiwazuia lakini kwa sasa wameshakua na wanamaamuzi ya kufanya mengi ndiyo maana unaona kwa sasa Asley anapost ana mtoto hiyo ni ishara ya kuonesha kuwa wameshakua” Alisema Chamuso.

Akimalizia amesema kwa sasa mashabiki wasubirie ngoma mpya na video nzuri kutoka kwa Yamoto Band kwa kuwa hamna tatizo lolote na uongozi wao na hakuna tatizo lolote baina yao.