Chaby Six kutimiza miaka 8 kwenye muziki kiaina yake

0

Rapa kutoka visiwani Zanzibar, Chaby Six ambaye hivi karibuni anatarajia kufanya onyesho lake la kutimiza miaka 8 tangu uwepo wake katika saana ya muziki ambapo amelipa jina la onyesho “Usiku wa Kimewaka”

chaby six

Akizungumza na Zenji255 Chaby amesema kuwa, ni muda mrefu toka kautumikia muziki na mpaka sasa alipofikia ni sehemu nzuri kwani umemsaidia mambo mengi ndani na nje ya Zanzibar.

“Kwa sasa nashukuru mungu mpaka hapa nilipofikia, Chaby six wa sasa sio yule aliyeanza muziki kipindi kile. Imefikia wakati na mimi niwe naongea na mashabiki wangu juu ya muziki na maisha yangu, na moja wapo ndio hili naanza nalo kwa kutimiza miaka 8 ya uwepo wangu katika muziki” Amesema Chaby Six.

Katika onyesho hilo litakalofanyika tarehe 30 Juni, Chaby Six anatarajiwa kusindikizwa na wasanii kama Abramy, Catty Soul, DJ Waiz, Madawa na muigizaji Ussi Haji.