Chaby Six Afiwa na Baba yake mzazi

0

Baba mzazi wa rapa kutoka visiwani Zanzibar Chaby Six Mashine, Mzee Mshimba, amefariki dunia Ijumaa hii.

chaby six

Akitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake Facebook, Chaby Six alisema mazishi yatafanyika leo Jumamosi (tar 1, Julai) saa nne asubuhi katika kijiji cha Bambi, Unguja.

Akizungumza na Zenji255 amesema, “Nipo katika wakati mgumu lakini namuomba Mungu anipe wepesi. Baba nilimpenda lakini amempenda zaidi. Namtakia safari njema na mungu amlaze mahala pema peponi” amesema.