Chaby Six aamua kuingia studio kutengeneza wimbo mpya

0

Baada ya kukaa kimya cha muda mrefu kilichozidi mwaka mzima, rapa Chab Six Mashine ambaye kwa hivi sasa anafanya kazi peke yake ameamua kuingia studio na kurekodi wimbo mpya ukiwa kama ujio wake mpya.

chaby six

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Chaby Six ameweka video inayoonyesha ana rap kwenye wimbo ambao tayari ushawekewa sauti yake.

Akiongea na Zenji255 Chaby amesema kuwa, baada ya kubanwa na majukumu mengi ya kifamilia na vile vile ndoa ilimkalia karibu ilibidi kwanza afanye mambo hayo na ndio ukimya uliomfanya akae muda mrefu bila ya kuachia wimbo wala kuingia studio yoyote kwa muda huo.

“Tayari nishatengeneza ngoma 2 katika studio za Action Records, lakini kwa sasa nitaizungumzia moja ambayo nimemshirikisha Issa RnB, jina bado haijapewa na ipo katika hatua za mwisho karibuni tu itakuwa hewani. Na safari hii Mashine inarudi kivyingine, ishapasishwa na imejaa spea mpya kutoka kiwandani” Alimalizia Chaby Six