(+Picha): Bunge Sports Club na Baraza la Wawakilishi zatoka sare ya bao 1-1 uwanja wa Amani Zanzibar

0

Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge Sports Club usiku wa leo Aprili 26, 2016 imeweza kutoka sare ya bao 1-1, dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan, Unguja na kushuhudiwa na watu mbalimbali.

image

Mchezo huo wa aina yake na wa kipekee kwa kikosi hicho cha Bunge Sports Club kiliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia wakati wote ambapo waliweza kupata bao lao la kuongoza ndani ya dakika 22 ya mchezo katika kipindi cha kwanza bao safi lililofungwa kwa kushuti la nje ya 18 na kuwaacha Wachezaji wa Baraza la Wawakilishi wasijue la kufanya.

image

Bao hilo la Bunge Sports Club ambalo lilikuwa la ushindi lilidumu hadi kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 67, Timu ya Baraza la Wawakilishi ilifanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya mchezo kuwa 1-1. Bao hilo lilipachikwa kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya hasa mvua kiasi cha kuwapoteza vibaya wachezaji wa timu ya Bunge ambao walicheza katika mazingira magumu sana.

Angalia picha za mechi hiyo.

image image image image image image image image image image image image image image image image image image image image image