“Bonge sijazinguana nae ila utaratibu wa kikazi ndio uliomsimamisha kufanya kazi nasi” – HK

0

Meneja wa Good father Music, Khamis HK amekanusha juu ya kauli zinazosambazwa kati yake na mtayarishaji wa muziki aliyekuwa akifanya kazi chini ya studio ya Minane, Bonge Jr kuwa wana uhasama baada ya Bonge Jr kuihama studio hiyo na kwenda kufanya kazi kwingine.

HKAkizungumza na Zenji255 HK anasema kuwa, hana ugomvi wala kinyongo na Bonge na tupo fresh tukionana ila kilichofanya tusielewane kwa muda ni kutokana na kukiuka masharti ya kazi ambayo tuliyokuwa tukifanya akiwa na Good father music.

“Mimi nipo fresh na Bonge na wala sijazinguana nae ila kilichonifanya nisimame kufanya nae kazi ni kutofuata utaratibu. Bonge alipata kazi sehemu nyingine wakati yupo chini ya uongozi Minane Empire, na wala hakutoa taarifa yoyote. Tulipomuuliza hasemi lolote, sasa na sisi tutafanyaje kama yeye hakuweza kutupa jibu sahihi” Amesema HK.

Zenji255 itamtafuta Bonge Jr kuzungumzia kuhusiana na hili, Endelea kutufuatilia ili tukujuze zaidi.