BMW aliyouliwa kwa risasi Tupac yauzwa zaidi ya shilingi bilioni 3

0

Gari ambayo aliyopigwa risasi rapa Tupac Shakur akiwa ndani sasa ipo mnadani na kuuzwa kwa dola milioni 1.5.

tupac

Gari hiyo ya BMW 1996 750iL iliyoweka historia kutokana na tukio hilo lililosababisha kifo chake, lipo mnadani kupitia kampuni ya MomentsInTime.com, ambapo dalali anaesimamia mauzo ya gari hiyo anaitwa Nick Alexander Imports.

Tupac kwa mara ya mwisho alipigwa risasi akiwa katika gari hiyo amekaa katika kiti cha abiria ambapo mmiliki wa studio ya Death Row Records Suge Knight akiwa amekaa kwenye usukani muda mfupi baada ya kupigwa picha za uchunguzi.

Tukio hilo ambalo mpaka leo bado halijapata ufumbuzi lilitokea jijini Las Vegas mnamo Septemba 7, 1996.