BET wataja list ya wasanii watakaotoa burudani siku ya tuzo hizo

0

Ikiwa imebakia siku kadhaa kuendea katika ugawaji wa tuzo za BET, imewataja wasanii watakaopanda katika steji siku ya tuzo ambapo akiwepo msanii kutoka Afrika katika orodha hiyo.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika katika jiji la (L.A) Los Angeles nchini Marekani katika ukumbi wa Microsoft Theater tarehe 25, Juni. Msanii tokea Nigeria Wizkid nae ametajwa katika watu watakaoshiriki kutoa burudani kwenye Tuzo hizo kubwa huku list hiyo ikiwa na wasanii nguli kama vile Snoop Dogg, Wiz Khalifa, Pusha T, Desiigner, Bryson Tiller, Rae Sremmurd, Jhené Aiko na New Edition.

Katika awamu ya kwanza BET wamewataja pia wasanii kama Migos, Bruno Mars, Future, Trey Songz na Tamar Braxton ndio watakaoanza kupanda kwenye stage kutoa burudani katika usiku huo.

Ambapo katika vipengele vya kugombania tuzo hizo, mwanadada Beyonce na Bruno Mars ndio walio ongoza kutajwa katika vipengele tofauti, Huku Beyonce akiwania vipengele saba, na Bruno Mars akiwania vipengele vitano.

Pia wasanii kama Solange, Chance the Rapper na Migos,wakiwa katika vipengele vinne vinne.