BE.TALENT: Hii hapa ni kwa ajili yako wewe mwenye kipaji

0

Lebo inayojihusisha na kusimamia wasanii wa muziki pamoja na kujishuhulisha na mambo ya kijamii, Stone Town Records imeandaa mashindano yanaoitwa BE.TALENT kwa ajili ya kutafuta vipaji katika sanaa tofauti.

Akizungumza na Zenji255 mkurugenzi wa lebo hiyo Mash Marley amesema kuwa, dhumuni la mashindano ni kuweza kuibua vipaji vipya katika sanaa tofauti ikiwemo muziki, uigizaji, uchekeshaji, dancers na nyinginezo.

“Kwa muda mrefu tulikuwa tuna malengo haya ya kufanya mashindano ila tulikuwa katika mipango ya kuweka kila kitu sawa. Zanzibar kuna vipaji vingi na tofauti, na tumeliona hili kupitia matukio mbali mbali ambayo kila siku huwa yanatokea hapa kwetu, kama vituo vingi vya habari huja Zanzibar kutafuta vipaji.” Amesema Mash.

Mash ameongezea kuwa “Kwa upande wetu sisi tukaona tusiangalie watangazaji tu, bali tuangalie pande zote ili mradi tuliwakilishe neno SANAA, Kiukweli tumejianda na kamati ipo vizuri tu hakutokuwa na upendeleo wowote”

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kwa maelezo zaidi endelea kufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ili kuweza kujua lini, wapi na muda gani yanafanyika mashindano hayo.

Kwa wale wanaotaka kushiriki katika mashindano bonyeza hapa kwa kuijaza fomu ya ushiriki.