(+Video): Baada ya kufungwa mechi zilizopita Barcelona yalipiza kisasi kwa Deportivo goli 8-0

0

kupokea vipigo kutoka vilabu vya Valencia, Atletico Madrid, Real Sociedad na kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Atletico Madrid, FC Barcelona wamerudi tena dimbani kucheza dhidi ya klabu ya Deportivo la Coruna.

Katika mchezo huo wa 34 kwa FC Barcelona wameonesha hasira na kuifunga Deportivo jumla ya goli 8-0, ushindi ambao umekuja siku chache baada ya kufungwa na klabu ya Valencia goli 2-1. FC Barcelona wameifunga Deportivo na kufikisha jumla ya point 79.

Magoli ya FC Barcelona yalianza kufungwa dakika ya 11 na 24 kupitia kwa Luis Suarez ambaye alifunga tena magoli mengine mawili dakika ya 53 na 64 baada ya Ivan Raktic kupachika goli la tatu dakika ya 47, Lionel Messi goli sita dakika ya 73 na Neymar akahitimisha kwa kufunga magoli mawili ya mwisho dakika ya 79 na 81.

kwa upande mwingine katika ligi hiyo hiyo ya Hispania wapinzani wa Barcelona, Real Madrid  ilicheza na Villareal CF ambapo Madrid walishinda 4-0. Wakati Atletico Madrid waliwafunga Athletic Club 1-0 na Valencia waliibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Eibar.

Video ya magoli ya mechi ya Deportivo vs FC Barcelona, Full Time 0-8