Balozi Seif Ali Iddi amesema elimu itolewe kwa viongozi wachanga

0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Viongozi wakuu wanajukumu la kuwaelimisha viongozi wachanga juu dhana halisi ya uwezo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .


Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo Ofisini kwake Vuga wakati akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mazigira George Simbachawene aliyefika kujitambulisha baada ya Kuteuliwa Hivi karibuni kushika Wadhifa huo.

Amesema kazi kubwa inayokabili Watanzania kwa wakati huu ni kuendelea kuuimarisha Muungano huo ulioleta faida kubwa Kiuchumi na Ustawi wa Jamii, faida ambayo inaweza kuwa funzo zuri la kuigwa na Mataifa mengine.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuhakikishia Waziri Simbachawene kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Ofisi yake katika Kazi kubwa iliyo mbele ya kuona Umoja na Mshikamano uliojengeka kupitia Muungano huo inaimarika na kustawi kwa maslahi ya Wananchi wote.

Mapema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mazigira George Simbachawene amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una shabaha Maalum iliyopelekea Waasisi wa Taifa hili kufikia mamuzi ya Kuunganisha Mataifa Mawili yaliyo Huru.