Baby J kuzindua Foundation yake ya kuwasaidia wasanii wa muziki Zanzibar

0

Msanii wa muziki kutoka Zanzibar Baby J Machi 18 anatarajia kufanya party maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa Foundation yake mpya ambayo itakuwa inajihusisha na kuwasaidia wasanii.

baby j

Akiongea na Zenji255 Baby J amesema kuwa siku hiyo ni siku muhimu kwake ambapo anatarajia kuonyesha ujio wake mpya kuanzia muziki hadi foundation anayotarajia kuanzisha baada ya shuhuli hiyo kuisha.

“Natarajia kuzindua Baby J Foundation na lengo kubwa na kufanya hivyo ni kuwasaidia wasanii wanaochipukia hasa hasa nimejikita kwa upande wa wasanii wa kike na ukimya wangu ulikuwa ni kufanya uchunguzi ni kitu kinachowasababishia watoto wa kike hawapati nafasi kwa hapa Zanzibar” Amesema Baby J.

Party hiyo imepangwa kufanyika Maruhubi Beach Villa, Maruhubi kuanzia saa moja usiku.