Baada ya kutolewa kwenye Dance100%, Kundi la ‘J Combat’ lapewa nafasi nyingine

0

Kundi la J Combat kutoka Zanzibar lililoshiriki Dance100% 2016 hadi nafasi ya nusu fainali na kutolewa, limerejeshwa baada ya kubainika kuwa lilishindwa kutokana na muda wa maandalizi katika wimbo mmoja haukuwa sawa ikilinganisha na makundi mengine.

j combatMeneja Mauzo na Masoko wa East Africa Television Bw. Roy Mbowe amesema uamuzi wa kurejesha kundi hilo umefikiwa baina ya waandaaji wa shindano EATV pamoja na BASATA baada ya kujiridhisha kwamba kuna umuhimu wa kurejesha kundi hilo ili kujenga usawa kwa washiriki wote.

“Imegindulika kwamba wimbo mmoja walifanya mazoezi kwa muda pungufu wa wiki moja ukilinganisha na makundi mengine ambayo yalifanya mazoezi kwa muda wa wiki mbili ambapo BASATA pia wamepitia jambo hilo na kwa pamoja tukaridhia kuwarejesha baada ya kuona wana sababu ya msingi” Amesema Roy.

Maamuzi ya kurejeshwa kwa kundi hilo yametangazwa leo mbele ya uwakilishi wa BASATA pamoja na makundi yote matano ambayo yalifuzu hatua ya fainali.

Kufuatia kundi hilo kurejeshwa katika fainali ya mwaka huu yatashiriki jumla ya makundi sita, ambapo mshindi atajinyakulia shilingi milioni 7.