Baada ya kufanya kazi na Barnaba, Mantuzo aelezea msanii anayefuata

0

Hit Maker wa furaha yangu ‘Mantuzo’ baada ya wimbo wake huo kufanya vizuri na mashabiki kuzikubali kazi zake, ameamua kufunguka na kusema msanii gani ambaye atakaependelea kufanya nae kazi nyingine.

mantuzo

“Kuna kazi nyingi zinakuja, tena za kufa mtu ile niliyofanya na Barnaba ni cha mtoto” Alisema Mantuzo.

Aliongeza kuwa “Kwa sasa project zangu ni kufanya kazi na ‘Masuper Star’ kutoka upande wa pili (Tanzania Bara) na nishafanya kazi na msanii mkubwa tu ambaye anafanya music kama anavyofanya Barnaba lakini siku haijafika kuweza kusema kwamba nimefanya na nani na ni mtu ambaye muziki wake unapendwa na kina dada na watoto ila muda ukifika nitasema ni msanii gani.”