(+Picha): Azam FC yatupwa nje michuano CAF

0

NDOTO za Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika zimefutika baada ya jana kufungwa na Esperance ya Tunisia mabao 3-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Olympique de Rades.

Azam FC kupoteza mchezo huo wa marudiano wa raundi ya pili ya michuano hiyo, kumeifanya itoke kwa kufungwa jumla ya mabao 4-2 na hii ni kufuatia awali timu hiyo kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam.

image image image image image image image image image image image image image image image

Picha na Azamfc.com